Contact Us | FAQ | Mails | Complaints |

FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA

Posted on: November 29th, 2019

FAHAMU KUHUSU HOMA YA EBOLA

Ugonjwa wa Homa ya Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi vya ebola. Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ya milipuko yajulikanayo kama homa za virusi vinavyo sababisha kutoka damu mwilini.

Kuna aina tano za virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ebola kama ifuatavyo; Zaire ebola virus, Sudan ebolavirus,Taï Forest ebolavirus, na Bundibugyo ebolavirus).Hivi vinasababisha ugonjwa wa Homa ya Ebola kwa binadamu.Kirusi cha tano kinaitwa Reston ebolavirus ambacho husababisha ugonjwa wa Ebola kwa wanyama peke yake

Ugonjwa huu kwa asili huanzia kwa wanyama kama vile nyani, kima sokwe na popo. Ugonjwa wa homa ya ebola huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu au binadamu kwa binadamu mwingine kwa njia ya haraka.


Jinsi ya ugonjwa wa homa ya ebola unavyoambukizwa toka kwa wanyama kwenda kwa binadamu

Binadamu anapata virusi vya ugonjwa wa homa ya Ebola kwa kula au kugusa viungo na majimaji ya wanyama pori wenye maambukizi ya ugonjwa huo.

Jinsi ya ugonjwa wa ebola unavyoambukizwa miongoni mwa jamii

 • Kugusa majimaji ya mwili kama vile damu, matapishi, jasho, mate, machozi, mkojo au kinyesi kutoka kwa mtu aliyeambukizwa na ugonjwa huo
 • Kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyeku fa kwa ugonjwa wa ebola
 • Kugusa vyombo na nguo zilizotumiwa na mtu mwenye maambukizi ya ebola
 • Kutumia vifaa vilivyotumika kum hudumia mgonjwa wa homa ya Ebola kama vile Sindano au Nyembe
 • Kujamiana na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Ebola

Ugonjwa huu hauenezwi kwa njia ya Hewa,Maji au Chakula

 

  Dalili za ugonjwa wa homa ya ebola                      

Dalili za ugonjwa wa homa ya ebola huanza kujitokeza kwa mtu aliyeambukizwa na virusi hivi kuanzia siku 2 hadi 21 tangu kupata maambukizi. Dalili hizo ni pamoja na:

 • Homa kali
 • Kulegea kwa mwili
 • Maumivu ya misuli
 • Kuumwa kichwa na vidonda kooni
 • Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha na vipele vya ngozi
 • Kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa na virusi
 • damu hutoka sehemu za wazi za mwili kama vile kwenye macho, pua, masikio, mdomo na njia za haja ndogo na kubwa

    Matibabu                                                                 

Ugonjwa wa homa ya ebola hauna tiba maalum wala chanjo, hata hivyo mgonjwa hutibiwa kulingana na dalili zitakazo ambatana na ugonjwa huo. Kuna uwezekano mkubwa wa  kuepuka mgonjwa kupoteza maisha iwapo mgonjwa huyo hatawahi kupata huduma stahiki.

  Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya ebola Ugonjwa wa homa ya ebola unaweza kuzuilika iwapo tutazingatia yafuatayo;

 • Epuka kugusa damu, matapishi, kamasi, mate, machozi, mkojo, kinyesi na majimaji yanayotoka kwenye mwili wa mtu mwenye dalili za ugonjwa wa homa ya ebola.
 • Epuka kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyekufa akiwa na dalili za ugonjwa wa homa ya ebola, toa taarifa kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kwa ushauri.
 • Epuka kutumia sindano,Kiwembe,m kasi,nguo, matandiko, kitanda, godoro na vyombo vilivyotumika na mtu mwenye dalili za ugonjwa wa homa ya ebola
 • Epuka kukutana kimwili na mtu mwenye dalili za ugonjwa wa homa ya Ebola
 • Epuka kugusa wanyama kama vile popo, nyani sokwe, tumbili na swala au mizoga ya wanyama.
 • Zingatia ushauri na maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya na viongozi wa serikali.
 • Wahi kituo cha kutolea huduma za afya unapohisi mojawapo ya dalili za ugonjwa wa ebola
 • Toa taarifa mapema kwenye kituo cha huduma za afya au kwa viongozi wa serikali ya mtaa, kijiji au kata mara uonapo mtu mwenye dalili za ugon jwa wa ebola.