Contact Us | FAQ | Mails | Complaints |

NJOMBE RRH KUANZISHA KLINIKI MAALUMU KWA WATOTO WENYE KISUKARI

Posted on: December 12th, 2023

Kliniki ya Ugonjwa wa Kisukari kwa watoto inatarajiwa kuanza hivi karibuni katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe baada ya tatizo  hilo kuonekana lipo nchini.

Uanzishwaji wa kliniki hiyo ni maazimio ya viongozi baada ya kikao cha uwasilishaji taarifa kuhusu ugonjwa huo, leo Desemba 13, 2023 ambapo Dkt. Onesmo Kitosi kutokea Idara ya Magonjwa ya ndani ndiye aliyewasilisha na kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa kisukari kwa watoto.

Dkt. Kitosi, ametoa elimu kuhusiana na chanzo cha Ugonjwa, dalili za ugonjwa huo, pamoja na vitu vya kuzingatia wakati wa utoaji huduma kwa mgonjwa.

Taarifa yake pia ilijikita katika takwimu zinazoonesha hali ya ugonjwa huo kwa Tanzania na duniani ambapo imeonesha kuwa asilimia 1.8 hadi 1.9


biliwa na Tatizo la Ugonjwa wa Kisukari huku Finland ikiwa ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na watoto wenye ugonjwa huo kwa asilimia 60.

  Ametoa wito kwa wananchi kutohusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina, kwa kile alichoeleza watu wengi kuamini kuwa ugonjwa wa kisukari unawapata watu wenye umri mkubwa tu, hivyo anapozaliwa mtoto na tatizo hilo, wengi wamebaki na nadharia ya kurogwa.

  Pia ameshauri wataalamu wa Maabara katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe kuanzisha huduma ya upimaji wa kisukari kwa watoto ili kuhakikisha usalama na uhakika wa afya kwa watoto wenye tatizo hilo mkoani Njombe na nchini kwa ujumla.

  Huduma hii itatolewa bure bila malipo yoyote kwa mtoto atakayechunguzwa na kugundulika ana ugonjwa wa Kisukari hadi pale atakapofikisha umri wa miaka 25.

  Elimu kuhusu ugonjwa wa Kisukari kwa watoto imetolewa leo ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Hospitali kutoa elimu kwa watumishi kila wiki ktuoka idara mbalimbali kwa lengo la kuongeza ujuzi, uzoefu na ufanisi mahali pa kazi.