Contact Us | FAQ | Mails | Complaints |

KAMPENI YA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA SARATANI

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani  Ocean Road inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe, Kutakuwa na huduma ya Uchunguzi na Matibabu ya Magonjwa ya Saratani kuanzia Tarehe 08-10/Aprili/2022  katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

Huduma zitakazotolewa ni

  • Elimu ya saratani
  • Uchunguzi wa awali wa saratani mbalimbali
  • Tiba kwa watakaogundulika na mabadiliko ya awali ya saratani hizo
  • Vipimo vya uchunguzi wa patholojia. 

- 04 April 2022